Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusudi La KirohoMfano

Kusudi La Kiroho

SIKU 1 YA 3

Kumjua Mungu hutuongoza katika utambuzi wa kina zaidi wa utambulisho wetu wa kiroho. Maarifa ya kina zaidi ya Mungu yanaweza kutuongoza kwenye ufahamu wa kina zaidi kujihusu sisi wenyewe kama wana na binti za Mungu.

Katika Yeremia 29:11 – 14, nabii Yeremia alikuwa akihutubia kundi la Waisraeli waliokuwa uhamishoni ambao walikuwa wameingiwa na majaribu ya kupoteza tumaini. Walielewa kwamba walikuwa wameshindwa na Wababiloni na kuhamishwa kutoka katika nchi yao kwa sababu ya dhambi yao, lakini walipaswa kufanya nini sasa? Wanapaswa kuishije maisha yao yote katika nchi hii ya kigeni? Walipoketi chini na kulia karibu na mito ya Babeli, waliuliza

“Tunawezaje kuimba wimbo wa Bwana katika nchi ya ugeni?” (Zaburi 137:1 – 4).

Waisraeli walikuwa wamesahau kwamba ingawa walihamishwa kutoka katika nchi yao, hawakufukuzwa kutoka kwa Mungu wao. Wao walikuwa bado ni watu wateule wa Mungu, na bado aliwafanyia ishara katikati ya hali zao ngumu ili wamtafute na kumjua kwa undani zaidi:

“Mtanitafuta na kunipata wakati mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nitaonekana kwenu” (Yeremia 29:13 – 14a).

Tunapolemewa na hisia kwamba maisha yetu hayana mwelekeo, ni lazima tukumbuke kwamba kipaumbele chetu cha kwanza kama watu wa Mungu kinapaswa kuwa kutafuta kumjua Mungu kwa ukaribu zaidi.

Wakati ujao unapojikuta umekwama katikati ya mwamba na mahali pagumu, badala ya kunung'unika kuhusu hali ambayo imekukabili, tafuta ufahamu wa kina wa Mungu.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kusudi La Kiroho

Tukiangalia maagizo ambayo Yeremia alitoa kwa watu waliohamishiwa Babeli, tunaweza kujifunza kweli zinazohusu kutafuta kusudi letu, na hilo tulilo kusudiwa kuwa kwa ajili ya Kristo. Mpango huu wa kusoma na Dk. Tony Evans...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha