Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuumbwa Kwa Desturi Na MunguMfano

Kuumbwa Kwa Desturi Na Mungu

SIKU 2 YA 3

Watu wengi sana hutumia maisha yao kujaribu kuwa mtu mwingine. Hii ndiyo sababu mimi huuliza kila wakati, "Kwa nini ujaribu kuwa mtu mwingine?" Mungu tayari ana mmoja wenu. Kuna mmoja tu - na wewe ndiye.

Mojawapo ya hatua za kwanza za kuishi kulingana na hatima yako inakuja kwa kutambua kuwa ni hatima YAKO. Mungu alikuumba uwe wa kipekee kwa makusudi. Ana mpango ambao ni utu wako, historia, tabia, mawazo, ujuzi na kila kitu kingine tu kinaweza kutimiza. Jikumbatie—acha kufanya ulinganisho mwingi. Sitisha mashindano. Acha wivu, kijicho au majuto. Kuwa kama vile ambavyo Mungu amekuumba uwe – kuwa wewe na utakuwa katika njia yako ya kudhihirisha ndani yako kusudi ambalo Mungu amekuumba ulitimize.

Mwombe Bwana akusaidie kukumbatia upekee wako. Acha akufunulie jinsi sifa hizi spesheli ambazo ni zako tu zinaweza kutumika kwa njia kuu unapoishi na kutekeleza hatima yako. Mshukuru Mungu kwa kukufanya kuwa tofauti, kwa sababu umeumbwa maalum.

Unapaswa kufanya nini unaposhawishiwa kujilinganisha na wengine?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Kuumbwa Kwa Desturi Na Mungu

Kila mmoja wetu ni wa kipekee. Hakuna mwingine kama wewe—na hakuna mwingine kama mimi. Hiyo si ajali. Ni mpango wa Mungu. Ana kusudi la kipekee kwako ambalo linategemea mtu wa kipekee aliyekuumba uwe. Acha mwandishi maar...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha