Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumchukua Mungu Kwa UzitoMfano

Kumchukua Mungu Kwa Uzito

SIKU 3 YA 3

Kuwa katika uhusiano wa agano na Mungu kunamaanisha kumchukulia kwa uzito.

Je, umewahi kusimama na ukafikiria kuhusu nguvu iliyo ndani ya gari lako? Bila kuingia kwenye mambo madogo madogo ya fizikia, wacha nitoe mfano rahisi sana. Mtu fulani amegundua kuwa ukigonga gari lako ukiwa unaendesha kwa mwendo wa maili 65 kwa saa, nguvu ya mgongano ni kama vile sawa na uliendesha gari lako lianguke kutoka kwenye jengo la orofa kumi na mbili.

Sasa, ikiwa kweli ulikuwa unaendesha gari letu juu ya jengo la ghorofa kumi na mbili, ungekuwa mwangalifu sana. Ila, kwa sababu tumezoea kuendesha gari kwa maili 65 kwa saa, wengi wetu hatufikirii jinsi inaweza kuwa hatari. Ukiondoa umakini wako barabarani, inaweza kuwa "mwisho wa mchezo."

Kuna mipaka inayouhusu matumizi ya gari lenye uwezo na nguvu nyingi. Tunachukua kuendesha gari kwa umakini na uzito.

Bado hata hivyo, wengi hawana fununu jinsi ya kufanya vivyo hivyo na Mungu. Wanataka faida za Mungu bila mipaka ambayo imeundwa na hofu na kicho kinachofaa. Wanamtendea Mungu kama askari wanayemwona kwenye kioo cha nyuma. Anaathiri kile unachofanya wakati anapokuwa karibu na kuonekana—labda kanisani au katika mpangilio wa ushirika wa kikundi kidogo. Lakini wakitoka nje ya utamaduni wa kikristo, na mguu unabonyeza kwa nguvu kiongeza kasi kwa mara nyingine tena.

Nini kinatokea tusipomchukulia Mungu kwa uzito?

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

Kuhusu Mpango huu

Kumchukua Mungu Kwa Uzito

Kwa sababu tumepata upendo na neema nyingi za Mungu, ni rahisi kuwa mlegevu kuhusu utii. Hatumchukulii Mungu kwa uzito vya kutosha. Tunaacha kumcha na hatuzingatii matokeo ya kutotii kwetu. Mruhusu mwandishi Tony Evans aambaye vitabu vyake vyauzwa sana akufundishe kuhusu baraka zinazotokana na kuweka agano na Mungu na hatari inayotokea tunapoacha kumchukulia kwa uzito.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative