Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 4 YA 31

Mungu anapenda rehema na haki. Kukosekana kwa rehema na haki kunaleta ubadhilifu. Wakristo tujihadhari tusiingie katika mtego wa kupokea takrima ambayo hupofusha macho. “Ujitie kisu kooni“, maana yake, zuia sana hamu yako, usije ukatumiwa na mvuto wa watu wenye hila. Kubali kufundishwa na Yesu Kristo. Anasema mioyo yetu itakuwa pale hazina yetu ilipo. Basi, weka tumaini lako katika hazina isiyoharibika. Kwa msisitizo Yesu anasema, Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu (Lk 12:33-34).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha