Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 27 YA 31

Tunalosoma hapa ni tukio la pekee. Ni nini hasa yaliyotokea usiku ule? Ni vigumu kueleza kikamilifu. Yakobo alishuhudia: Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka (m.30). Kwa hiyo yule mtu aliyekuja kushindana naye ni Mungu mwenyewe! Alikutana na Hofu ya Isaka, Mtakatifu! Na Yakobo alishinda (m.28, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda)! Kwa jinsi gani? Badala ya kuangamizwa kutokana na dhambi zake akapata msamaha, akabarikiwa (m.26 na 29, Sikuachi, usiponibariki. … Akambariki huko). Yakobo akashinda, akilia na kumsihi Mungu, imeaelezwa katika Hos 12:4. Hii ni hali ya toba na unyenyekevu inayompendeza Bwana (unaweza kutafakari zaidi jambo hili kwa kusoma Isa 57:15-19).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/