Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

SIKU 1 YA 30

Kazi ya malaika wenye nguvu ni kutangaza hukumu ya mwisho duniani. Mamlaka ya malaika huyu yanagusa uumbaji wote. Namba 7 inahusika na ukamilifu wa tukio lenyewe, yaani ... siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii. Hukumu hii inapotokea, ndipo kweli ya Mungu itajidhihirisha kwa dhahiri kuliko sasa, kama alivyoambiwa Danieli: Maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho (Dan 12:9). Wakati halisi hatuujui. Anaujua Kristo mwenyewe. Mungu ametufunulia jinsi ya kuishi sasa kwa njia ya Neno lake. Tusiyoyajua sasa tusubiri kwa imani. Mungu atayaweka bayana kwa wakati wake unaofaa. Hapo ndipo mwisho wa mambo yote utatokea.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu u...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha