Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu AnanipendaMfano

Jesus Loves Me

SIKU 2 YA 7

Zipi Muhimu?


Muhimu ni mafunzo za kimsingi za Kristo. Ondoa mojawapo, na nyumba ya Ukristo inaporomoka. Ni muhimu kwani ukipoteza mojawapo, unapoteza nguvu ya Kristo kukubadili. Kanisa ikipoteza mojawapo, inapoteza nguvu ya Mungu ya wokovu kubadili watu wake na jamii yake. 



Neno la Mungu linatoa hizi dhana muhimu—Maandiko ni uti wa mgongo wa imani hizi. Kichocheo chetu ni kujua imani za kimsingi za Ukristo kwa sababu vita vinaendelea ili kushinda roho zetu. Vita hivi kati ya wema na uovu vinapiganwa katika ulimwengu wa dhana—Udhahiri wa imani zako ni ala itakayokuwezesha kutofautisha kati ya dhana njema na dhana zinazopotosha au kulaghai. Kwa sababu tunapata nguvu na uzima wa Kristo kupitia imani yetu, sharti imani zetu ziwe sahihi.



Mstari wa kwanza wa wimbo upendwao, “Yesu Anipenda,” inaonyesha dhana za kimsingi za Ukristo:



Yesu / Anipenda / Mimi / Kweli ninajua / Kwani Biblia inasema.



Ukristo ni rahisi katika kiini chake ikiwa tunajua maana ya maneno hayo. Tumia njia hii kuuelewa:



YESU—Ninachoamini kuhusu Yesu



Yesu ni Mungu kikamili na binadamu kikamili, Masihi.



PENDA—Ninachoamini kuhusu upendo wa Mungu, alivyothibiti msalabani



Yesu alikuja ulimwenguni kwetu kwa utume wa kuokoa. Alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kutoka mautini.



MIMINinachoamini kujihusu



Kila mwanadamu ana utukufu—na pia ana uharibifu. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu lakini dhambi imetunajisi. Penye uovu imetufisidi, Yesu anaweza kuturejesha ili tuwe “kiumbe kipya.”



NINAJUANinachoamini ili kuwa na uhakikisho kuhusu wokovu wangu



Hatuwezi kustahili wokovu, lakini lazima tutumie nafsi yetu kukiri uhitaji wetu (tubu), kubali Yesu kuwa Mungu, na kuamini kazi yake msalabani. 



KWANI BIBLIA INASEMA—Ninachoamini kuhusu masharti ya Mungu kwa maisha yangu



Tunachagua Biblia kuwa kipimo kisichobadilika kwa yote tutendayo na kuamini kwani Yesu ni mfano wetu. Lazima tusome na kutii Neno la Mungu ili kutimiza utambulisho wetu katika Kristo.



Kwa kupitia vishazi vitano vya maneno ya wimbo huu, tunapata ala ya nguvu ya ukumbusho ya kubeba dhana muhimu za Ukristo popote tuendapo.






Sala: Fumbua macho na moyo wangu katika safari hii. Nisaidie kupokea ukweli huu kutoka Neno lako. Ninataka fikra zangu zigeuzwe. Nisaidie kuamini unachotaka niamini. Amina.  


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Jesus Loves Me

Ikiwa mtu angekuuliza, "Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?" ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, "Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuel...

More

Tungependa kushukuru Baker Publishing kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://bakerbookhouse.com/products/235847

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha