Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Tumaini Linaloishi: Hesabu kuelekea PasakaMfano

Living Hope: A Countdown to Easter

SIKU 2 YA 3

"Jipe moyo."



Biblia haituambii sana kuhusu muda kati ya kifo cha Yesu na ufufuko. Lakini, tunajua kwamba illitokea wakati wa sherehe ya Pasaka: sikukuu ya juma zima kukumbuka wakati Mungu alipowakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani.



Wakati wa sherehe, Wayahudi walishiriki chakula cha pamoja na sadaka safi ya mwanakondoo hekaluni kabla ya kuandaa pumziko la siku ya Sabato. Ilikuwa ni siku kabla ya Sabato ambapo mwili wa Yesu uliwekwa kaburini.



Fikiria wewe ni mwanafunzi wa Yesu wakati hili likitokea. Sio tu kwamba rafiki yako wa karibu ameuwawa kimakosa, bali pia hauruhusiwi kuomboleza kifo chake mpaka siku ya mapumziko itakapokwisha.



Kitu ambacho wanafunzi wa Yesu hawakujua wakati ule ni kuwa maumivu waliyokuwa wanayapitia yalikuwa sehemu ya hadithi kubwa—mpango wa kutukomboa sisi sote. Mungu aliuona ufufuko ukija, japokuwa wanafunzi hawakuuona.



Pumziko linatukumbusha kwamba Mungu ni Bwana wa hali zote. Na pumziko linatusaidia kuzingatia kilicho muhimu zaidi: Yule anayeahidi kutupatia yote tunayohitaji. Tunapochagua kutulia katikati ya magumu, tunachagua kumuabudu Mungu.



Kwa hiyo haijalishi nini kinaendelea kati yako leo, chagua kupumzika kwa Mungu—hata kama dunia imechagua kuwa na hofu. Hakuna lisilowezakana Kwake.



Omba:Yesu, leo, nisaidie kupumzika ndani Yako. Najua ya kuwa wewe ni mkuu kuliko chochote kinachoendelea kati yangu, Tumaini langu ni Wewe pekee kwa sababu Wewe ni wokovu wangu. Ninaamini kwamba tayari umejibu kilio cha moyo wangu, japokuwa bado nasubiri kuyaona majibu. Kwa hiyo leo, nachagua kukutazama Wewe. Katika jina Yesu, Amina.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Living Hope: A Countdown to Easter

Giza linapokuzunguka, ulikabili namna gani? Kwa siku 3 zijazo, zama katika hadithi ya Pasaka na ugundue jinsi ya kushikilia tumaini pale unapojisikia kuachwa, mpweke au usiye wa thamani.

Mpango huu wa asili wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha