Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 1 YA 7

Unashangaa kama maisha yako yanaelekea sehemu sahihi? 



Unapofikia umri wa miaka 18, unajisikia kwamba unatakiwa kuwa mtu mzima ghafla na kuanza maisha yako. Lakini inakuwaje unapokuwa na maswali mengi kuliko majibu? Unapojisikia kwamba hufikii matarajio yako uliojipangia au ya watu wengine? Wakati unaopoona ulipofikiria ungekuwa sipo ulipo sasa, na huna uhakika unakoelekea?



Hebu tulia. Tahadhari ya mharibu- hakuna ambaye anayajua maisha yake, lakini hilo ndilo muhimu. Sote tunajifunza kumtegemea Mungu na watu wengine wanaotuzunguka ili kuishi hatua moja kila siku. Kiukweli, Yesu alisema tusisumbuke kuhusu kesho kwa sababu siku yatosha kwa masumbufu yake.



Hiyo ni kweli? Tunapoanza kufikiria kuhusu fedha na maisha yetu ya baadaye na kazi zetu na mahusiano yetu- inakuwa ni mzigo. Lakini tunapotulia na kuiangalia siku moja kwa wakati, tunaanza kuondoa shinikizo kwetu na kuanza kumwangalia Mungu.



Hapa kuna jambo kuhusu maisha. Ni fupi sana. Hiyo inaonekana kama msongo, lakini Zaburi 90:12 inasema kujifunza kuzihesabu siku zetu hutuletea hekima. Ya ajabu? Siyo sana. Tunapotambua kwamba hatujaahidiwa kesho, tunaiona siku kama zawadi kutoka kwa Mungu. Zawadi iliyojaa rehema mpya. Neema mpya. Na nafasi zaidi ya kujifunza na kukua.



Kwa hiyo, kama unajiuliza kama maisha yako yanaelekea kunakostahili, hauko peke yako. Kama wanadamu, tuna tabia ya kutafuta majibu zaidi wakati tunachohitaji ni Mungu zaidi.



Lakini ni swali sahihi. Hata wakati wa siku za Yesu, watu waikuwa wanauliza maswali mazito. Kuna mmoja siku moja alimuuliza amri iliyo kuu ni ipi.



Yesu alichosema kilikuwa ni rahisi sana lakini kigumu sana. Alisema kilicho cha muhimu kufanya ni kumpenda Mungu na kuwapenda watu. Wakati mwingine, Yesu alisema ulimwengu utawatambua wafuasI wake kwa jinsi wanavyowapenda wengine.



Ni heri kusema, kama unampenda Mungu na kuwapenda watu wanaokuzunguka, yawezekana uko katika njia sahihi.



Kwa siku chache zijazo, tutaangalia baadhi ya maswali ya kikubwa ambayo wote tunakuwa nayo mara kwa mara na kuona jinsi Yesu anavyokutana nasi katikati ya maisha yetu ya kawaida kwa namna isiyokuwa ya kawaida.



Fikiri: Ni kwa njia zipi naweza kumpenda Mungu na watu wanaonizunguka?



Omba: Mungu, asante kwa kuwa wewe ni muweza na naweza kukutwika fadhaa zangu zote kuhusu yajayo. Asante kwa neema yako, rehema, na upendo wako. Nisaidie kukutegemea - siyo juhudi zangu mwenyewe. Nifundishe kuzihesabu siku zangu na kuutumia vizuri muda wangu mfupi duniani. Nisaidie kukupenda na kuwapenda wengine zaidi kila siku. Katika jina la Yesu. Amen.  



Unataka kujua zaidi juu ya kuwa kijana? Angalia mafundisho ya video inayofuata yenye sehemu 5Collective. 


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pam...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha