Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANEMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

SIKU 1 YA 7

  

KUJIGEUZA KWA YESU

28 Yapata siku nane baada ya Yesu kusema hayo, aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana akaenda nao mlimani kuomba.

Alipokuwa akiomba, mwonekano wa sura yake ukabadilika, mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi.Ghafula wakawaona watu wawili, Mose na Eliya wakizungumza naye.Walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea huko Yerusalemu.

32 Petro na wenzake waliokuwa wamelala usingizi mzito walipoamka,

wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.

33 Mose na Eliya, walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Yesu,

“Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu, kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” Lakini Petro alikuwa hajui asemacho.

34 Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu.Sauti ikatoka kwenye lile wingu ikisema,

“Huyu ni Mwanangu mpendwa niliyemchagua, msikilizeni yeye.”

36 Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Yesu akiwa peke yake.

Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyokuwa wameyaona.

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchangany...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha