Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3

SIKU 6 YA 7

Yesu amwita Matayo  

Yesu alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru.

“Nifuate.” Yesu akamwambia, Mathayo akaondoka, akamfuata.

"Wakati Yesu alipokuwa ameketi chakulani ndani ya nyumba, watoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja kula pamoja naye na wanafunzi wake.

Mafarisayo walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini Mwalimu wenu anakula na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

Lakini Yesu aliposikia hayo, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 3

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha