Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ondoa uogaMfano

Get Rid Of Fear

SIKU 1 YA 3

Uko tayari kujifunza jinsi ya kuiangusha ngome ya hofu ambayo adui ameijenga moyoni na akilini mwako? Yesu alikupa jibu. Unaiangusha kwa kubadili umuhimu. Hiki ndicho alikuwa anakiongelea katika Mathayo 6:33 aliposema, “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.



Kwa maneno mengine, kama utatumia muda wako na nguvu yako kukingana na Mungu anachokifanya katika kuendeleza ufalme wake duniani, amekuahidi kukuzidishia mambo yote ambayo yanakutia hofu. Yesu alisisitiza hayo aliposema “Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” (mstari 34).



Mungu anakupa neema kila siku. Hatakupa neema ya kesho leo, huihitaji. Kwa nini? Kwa sababu neno lake linatuambia, “Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.”(Ombolezo 3:22–23). Kwa hiyo kama unaogopa na hujui kitakachotokea kesho, ki msingi unamwambia Mungu kwamba humuamini. Unamwambia kwamba haaminiki. Na unapelekea mawazo yako kuwa mzunguko wa maumivu na hofu ambayo itaendeleza tabia yako badala ya kukusaidia kushinda. Kuogopa mambo ya kesho ni kukosa amani na ushindi leo. Acha hofu iondoke.



Bwana wa neema, nisaidie kutambua hofu inapoinuka mawazoni mwangu. Nisaidie kuyateka mawazo haya kabla hayajaongezeka na kukua. Nipe hekima kutambua kilicho kweli na kisicho kweli, na katika yote niwezeshe kuamini kwamba upo pamoja nami. Napenda kukutwika wewe fadhaa zangu, tafadhali naomba neema kufanya hivyo leo na kila siku. Katika jina la Yesu. Amen.



Umefurahia masomo haya ya kila siku na maombi? Tunapenda kukutia moyo na zawadi ya mahubiri matatu ya Tony Evans kwa kupakua kwenye kiunganishi hiki, ambayo yanaenda ndani zaidi ya tulichojadili leo. Just visit the link here.  
siku 2

Kuhusu Mpango huu

Get Rid Of Fear

Unaweza kushinda hisia za uoga. Dk. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu maalum. Vumbua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukiyasubiri unapotumia kanuni zinazoletwa na mpango huu

Tungependa kushukuru Harvest House Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://go.tonyevans.org/addiction

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha