Tito 3:9-11
Tito 3:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini jiepushe na ubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishano juu ya sheria. Mambo hayo hayana faida yoyote na ni ya bure tu. Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye. Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake zathibitisha kwamba amekosea.
Tito 3:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu. Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye; maana unajua ya kuwa mtu kama huyo ni mpotovu na mtenda dhambi, naye amejihukumia hatia yeye mwenyewe.
Tito 3:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
Tito 3:9-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi, mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu sheria, kwa sababu hayana faida, tena ni ubatili. Mtu anayesababisha mafarakano, mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena. Kwa kuwa unajua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi. Yeye amejihukumu mwenyewe.