Tito 3:12-13
Tito 3:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi. Jitahidi kumsaidia mwanasheria Zena na Apolo ili waweze kuanza ziara zao, na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji.
Tito 3:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi uwezavyo kujiunga nami katika Nikopoli; kwa kuwa nimekusudia kukaa huku wakati wa baridi. Jaribu uwezavyo kumsaidia Zena, yule mwanasheria, na Apolo, ili wakiwa safarini wasipungukiwe na chochote.
Tito 3:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi. Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote.
Tito 3:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi. Fanya kila uwezalo uwasafirishe Zena yule mwanasheria na Apolo na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji katika safari yao.