Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tito 3:1-3 - Compare All Versions

Tito 3:1-3 BHN (Biblia Habari Njema)

Wakumbushe watu kuwastahi watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila namna kutenda mambo yote mema. Waambie wasimtukane mtu yeyote; bali waishi kwa amani na masikilizano, wawe daima wapole kwa kila mtu. Maana, wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu, wakaidi na wapotovu. Tulikuwa watumwa wa tamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha ya uovu na wivu; watu walituchukia nasi tukachukiana.

Shirikisha
Tito 3 BHN

Tito 3:1-3 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakiwa wapole sana kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

Shirikisha
Tito 3 SRUV

Tito 3:1-3 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

Shirikisha
Tito 3 SUV

Tito 3:1-3 NEN (Neno)

Wakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na kwa wenye mamlaka, na kutii, wakiwa tayari kutenda kila lililo jema, wasimnenee mtu yeyote mabaya, wasiwe wagomvi bali wawe wema, wakiwa wapole kwa watu wote. Maana sisi wenyewe wakati fulani tulikuwa wajinga, wasiotii, tukiwa watumwa wa tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tuliishi katika uovu na wivu, tukichukiwa na kuchukiana sisi kwa sisi.

Shirikisha
Tito 3 NEN