Ruthu 1:20-21
Ruthu 1:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Naomi akasema, “Msiniite tena Naomi niiteni Mara, kwa maana Mungu mwenye nguvu ameyafanya maisha yangu yawe machungu mno. Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.”
Ruthu 1:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
Ruthu 1:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
Ruthu 1:20-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Akawaambia, “Msiniite tena Naomi; niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi amenitendea mambo machungu sana. Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? BWANA amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”