Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Rut 1

1
Familia ya Elimeleki Yaenda Moabu
1 # Amu 2:16; Mwa 12:10; 26:1; Kum 28:38; 1 Fal 18:2; 2 Fal 8:1; Amu 17:8; Mik 5:2 Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2#Mwa 35:19; Amu 3:30Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. 5Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.
Naomi na Wakweze Wamoabi
6 # Kut 4:31; Zab 80:14; Yer 29:10; Sef 2:7; Zek 10:3; Lk 1:68; 7:16; Mwa 28:20; 48:15; Kut 16:4,6; Zab 104:14,16; Mit 30:8; Isa 55:10; Mt 6:11 Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika nchi ya Moabu amesikia ya kwamba BWANA amewajilia watu wake na kuwapa chakula. 7Basi akatoka pale alipokuwapo, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda. 8#Yos 24:15; 2 Tim 1:16Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia. 9#Rut 3:1BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. 10Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. 11#Mwa 38:11; Kum 25:5Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? 12Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; 13#Amu 2:15; Ayu 19:21; Zab 32:4; 38:2je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu. 14#Kum 4:4; 10:20; Mit 17:17; 18:24; Yn 6:66-69; Ebr 10:39Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye. 15#Yos 24:15-21; Amu 11:24Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako. 16Naye Ruthu akasema,
Usinisihi nikuache,
Nirejee nisifuatane nawe;
Maana wewe uendako nitakwenda,
Na wewe ukaapo nitakaa.
Watu wako watakuwa watu wangu,
Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17 # 1 Sam 3:17; 25:25; 2 Fal 6:31 Pale utakapokufa nitakufa nami,
Na papo hapo nitazikwa;
BWANA anitende vivyo na kuzidi,
Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
18 # Mdo 21:14 Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye.
19 # Mt 21:10; Isa 23:7; Omb 2:15 Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20Akawaambia, Msiniite Naomi#1:20 Naomi maana yake ni, Kupendeza., niiteni Mara#1:20Mara maana yake ni, Uchungu., kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. 21#1 Sam 2:7,8; Ayu 1:21Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? 22#Kut 9:31; 2 Sam 21:9Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.

Iliyochaguliwa sasa

Rut 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha