Waroma 9:24-33
Waroma 9:24-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine. Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: “Wale waliokuwa ‘Si watu wangu’ nitawaita: ‘Watu wangu!’ Naye ‘Sikupendi’ ataitwa: ‘Mpenzi wangu!’ Na pale walipoambiwa: ‘Nyinyi si wangu’ hapo wataitwa: ‘Watoto wa Mungu aliye hai.’” Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaza sauti: “Hata kama wazawa wa Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaookolewa; maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya ulimwengu wote.” Ni kama Isaya alivyosema hapo awali: “Bwana wa majeshi asingalituachia baadhi ya watoto wa Israeli, tungalikwisha kuwa kama Sodoma, tungalikwisha kuwa kama Gomora.” Basi tuseme nini? Watu wa mataifa ambao hawakutafuta wafanywe waadilifu, wamejaliwa kuwa waadilifu, kwa njia ya imani, hali watu wa Israeli ambao walitafuta sheria ya kuwafanya kuwa waadilifu, hawakuipata. Kwa nini? Kwa sababu walitegemea matendo yao badala ya kutegemea imani. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Tazama, nitaweka huko Siyoni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Lakini atakayemwamini hataaibishwa!”
Waroma 9:24-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na kumwita mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai. Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa. Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata. Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora. Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikia ile sheria. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo, kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Waroma 9:24-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai. Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa. Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata. Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora. Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo, kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Waroma 9:24-33 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivi vyombo ni sisi, ambao pia alituita, sio kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa. Kama alivyosema Mungu katika Hosea: “Nitawaita ‘watu wangu’ wale ambao si watu wangu; nami nitamwita ‘mpendwa wangu’ yeye ambaye si mpendwa wangu,” tena, “Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ” Isaya anapaza sauti na kusema kuhusu Israeli kwamba: “Ingawa idadi ya Waisraeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki yao tu watakaookolewa. Kwa kuwa Bwana ataitekeleza hukumu yake duniani kwa haraka na kwa ukamilifu.” Ni kama vile alivyotabiri Isaya, akisema: “Kama Bwana wa majeshi hakutuachia uzao, tungekuwa kama Sodoma, tungefanana na Gomora.” Kwa hiyo tuseme nini? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kupitia kwa imani. Lakini Israeli, ambao walijitahidi kupata haki kupitia kwa sheria, hawakuipata. Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kupitia kwa imani bali kupitia kwa matendo. Wakajikwaa kwenye lile “jiwe la kukwaza”. Kama ilivyoandikwa: “Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu na mwamba wa kuwaangusha. Yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe”.