Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Rum 9

9
Mungu Ateua Israeli
1Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu, 2ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. 3#Kut 32:32Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; 4#Kut 9:4; Kut 4:22; Kum 7:6; 14:1,2ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; 5#Rum 1:25; Mt 1:1; Lk 3:23; Yn 1:1ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina. 6#Rum 2:28; Hes 23:19Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. 7#Mwa 21:12Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; 8#Gal 4:23yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao. 9#Mwa 18:10Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. 10#Mwa 25:21Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, 11(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye), 12#Mwa 25:23aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. 13#Mal 1:2-3Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14 # Kum 32:4 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! 15#Kut 33:19Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 16#Efe 2:8Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu. 17#Kut 9:16Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18#Kut 4:21; 7:3; 9:12; 14:4,17Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
Ghadhabu na Neema ya Mungu
19Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20#Isa 29:16; 45:9La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? 21#Yer 18:6Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22#Yer 50:25Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; 23#Efe 1:3-12; Rum 2:4; 8:29tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; 24ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? 25#Hos 2:23Ni kama vile alivyosema katika Hosea,
Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu,
Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
26 # Hos 1:10 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa,
Ninyi si watu wangu,
Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
27 # Isa 10:22-23; Rum 11:5 Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema,
Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa.
28Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.
29 # Isa 1:9 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena,
Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao,
Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.
Kutoamini kwa Israeli
30 # Rum 10:20 Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; 31#Rum 10:2,3bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria. 32#Isa 8:14Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo, 33#Isa 28:16; Mt 21:42; 1 Pet 2:6kama ilivyoandikwa,
Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao;
Na kila amwaminiye hatatahayarika.

Iliyochaguliwa sasa

Rum 9: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha