Waroma 9:24-26
Waroma 9:24-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine. Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: “Wale waliokuwa ‘Si watu wangu’ nitawaita: ‘Watu wangu!’ Naye ‘Sikupendi’ ataitwa: ‘Mpenzi wangu!’ Na pale walipoambiwa: ‘Nyinyi si wangu’ hapo wataitwa: ‘Watoto wa Mungu aliye hai.’”
Waroma 9:24-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na kumwita mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
Waroma 9:24-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
Waroma 9:24-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivi vyombo ni sisi, ambao pia alituita, sio kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa. Kama alivyosema Mungu katika Hosea: “Nitawaita ‘watu wangu’ wale ambao si watu wangu; nami nitamwita ‘mpendwa wangu’ yeye ambaye si mpendwa wangu,” tena, “Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ”