Waroma 9:23-25
Waroma 9:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake. Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine. Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: “Wale waliokuwa ‘Si watu wangu’ nitawaita: ‘Watu wangu!’ Naye ‘Sikupendi’ ataitwa: ‘Mpenzi wangu!’
Waroma 9:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na kumwita mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
Waroma 9:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
Waroma 9:23-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake? Hivi vyombo ni sisi, ambao pia alituita, sio kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa. Kama alivyosema Mungu katika Hosea: “Nitawaita ‘watu wangu’ wale ambao si watu wangu; nami nitamwita ‘mpendwa wangu’ yeye ambaye si mpendwa wangu,”