Waroma 16:25 - Linganisha Matoleo Yote
Waroma 16:25 BHN (Biblia Habari Njema)
Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya Yesu Kristo, na katika ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi zilizopita.
Waroma 16:25 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele
Waroma 16:25 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na Injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele
Waroma 16:25 NEN (Neno)
Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale.