Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Rum 16

16
Salamu za Kibinafsi
1Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; 2kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
3 # Mdo 18:2,18,26 Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; 4waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. 5#1 Kor 16:15,19Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. 6Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu. 7#2 Kor 8:23Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. 8Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. 9Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. 10Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. 11Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. 12Nisalimieni Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana. 13#Mk 15:21Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia. 14Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao. 15Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao. 16#1 Kor 16:20; 1 Pet 5:14Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.
Maagizo ya Mwisho
17 # Mt 7:15; Tit 3:10 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. 18#Flp 3:19; Eze 13:18; Kol 2:4; 2 Pet 2:3Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. 19#Rum 1:8; Mt 10:16; 1 Kor 14:20Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20#Rum 15:33; Mwa 3:15Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
21 # Mdo 16:1; 19:22; 20:4; Flp 2:19 Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu. 22Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. 23#Mdo 19:29; 1 Kor 1:14; 2 Tim 4:20Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji, awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.
[ 24Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.]
Sifa kwa Mungu
25 # Efe 1:9; 3:5,9; Kol 1:26 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, 26#2 Tim 1:10; Rum 1:5ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. 27#1 Tim 1:17; Yud 1:25Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Rum 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha