Waroma 12:9-11
Waroma 12:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
Waroma 12:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana
Waroma 12:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana
Waroma 12:9-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema. Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine. Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.