Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 6:12-13 - Compare All Versions

Ufunuo 6:12-13 BHN (Biblia Habari Njema)

Kisha nikatazama, na wakati Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi; jua likawa jeusi kama gunia la manyoya; mwezi wote ukawa mwekundu kama damu; nazo nyota za mbingu zikaanguka juu ya ardhi kama matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali.

Shirikisha
Ufunuo 6 BHN

Ufunuo 6:12-13 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

Shirikisha
Ufunuo 6 SUV

Ufunuo 6:12-13 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Nami nikaona, alipoufungua mhuri wa sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

Shirikisha
Ufunuo 6 SRUV

Ufunuo 6:12-13 NEN (Neno)

Nikatazama alipouvunja ule muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la ardhi, na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa singa za mbuzi, na mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. Nyota zilizo angani zikaanguka ardhini kama vile matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali.

Shirikisha
Ufunuo 6 NEN