Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 6

6
Mihuri saba
1 # Ufu 4:6; 5:1,2,6,8 Kisha nikaona Mwana-kondoo alipofungua mojawapo ya ile mihuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! 2#Zek 1:8; 6:3,6 Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, huku akishinda tena apate kushinda.
3Na alipoufungua mhuri wa pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! 4#Zek 1:8; 6:2 Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda aliruhusiwa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
5 # Zek 6:2,6 Na alipoufungua mhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. 6Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.
7Na alipoufungua mhuri wa nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! 8#Eze 5:12; 14:21; 29:5; 33:27; 34:28; Hos 13:14; Yer 15:3 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.
9 # Ufu 8:5; 14:18; 16:7 Na alipoufungua mhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10#Zek 1:12; Zab 79:10; Kum 32:43; Mwa 4:10; 2 Fal 9:7; Hos 4:1 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11#Ufu 3:4; 7:9; Mt 23:32 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wasubiri bado muda mchache, hadi itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu zao, watakaouawa kama wao walivyouawa.
12 # Ufu 11:13; 16:18; Isa 13:10; Yoe 2:10,31; 3:15; Mt 24:29; Mk 13:24-25; Lk 21:25; Eze 32:7,8 Nami nikaona, alipoufungua mhuri wa sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13#Isa 34:4; 13:10 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14#Ufu 16:20 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15#Isa 2:10,19,21; 24:21; 34:12; Yer 4:29; Zab 48:4; 2:2 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na muungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16#Hos 10:8; Lk 23:30; Isa 6:1; Zab 47:8 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwenye hasira ya Mwana-kondoo. 17#Yoe 2:11,31; Mal 3:2; Sef 1:14,18; Rum 2:5 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kuistahimili?

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 6: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha