Zaburi 78:67-72
Zaburi 78:67-72 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini aliikataa jamaa ya Yosefu, wala hakulichagua kabila la Efraimu. Ila alilichagua kabila la Yuda, mlima Siyoni anaoupenda. Alijenga hapo hekalu lake kubwa kama mbingu, kama dunia aliyoiweka imara milele. Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo. Alimtoa katika kazi ya kuchunga kondoo na wanakondoo, awe na jukumu la kuchunga watu wa Yakobo taifa lake. Achunge Israeli, watu wake Mungu mwenyewe. Daudi akawafunza kwa moyo wake wote, akawaongoza kwa uhodari mkubwa.
Zaburi 78:67-72 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ila akaikataa hema ya Yusufu; Wala hakuichagua kabila la Efraimu. Bali aliichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni alioupenda. Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele. Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake. Akawahudumia kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.
Zaburi 78:67-72 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ila akaikataa hema ya Yusufu; Wala hakuichagua kabila ya Efraimu. Bali aliichagua kabila ya Yuda, Mlima Sayuni alioupenda. Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele. Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake. Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.
Zaburi 78:67-72 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo alipoyakataa mahema ya Yusufu, hakulichagua kabila la Efraimu, lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele. Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake. Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.