Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 78

78
Wema wa Mungu na Israeli Kukosa Shukrani
Utenzi wa Asafu.
1 # Kut 19:5; Kum 32:29 Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
2 # Zab 49:4; Mt 13:35 Na nifunue kinywa changu kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya kale.
3 # Zab 44:1 Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,
Ambayo baba zetu walituambia.
4 # Kum 4:9; Kut 12:26; Yos 4:6,7 Hayo hatutawaficha wana wao,
Huku tukiwaambia kizazi kingine,
Sifa za BWANA, na nguvu zake,
Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
5Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo,
Na sheria aliiweka katika Israeli.
Aliyowaamuru baba zetu
Wawajulishe wana wao,
6 # Zab 102:18 Ili kizazi kingine wawe na habari,
Ndio hao wana watakaozaliwa.
Wasimame na kuwaambia wana wao
7Wamwekee Mungu tumaini lao.
Wala wasiyasahau matendo ya Mungu,
Bali wazishike amri zake.
8Naam, wasiwe kama baba zao,
Kizazi cha ukaidi na uasi.
Kizazi kisichojitengeneza moyo,
Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
9Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde,
Walirudi nyuma siku ya vita.
10Hawakulishika agano la Mungu;
Wakakataa kuenenda katika sheria yake;
11 # Isa 17:10; Yer 2:32 Wakayasahau matendo yake,
Na mambo yake ya ajabu aliyowaonyesha.
12 # Mwa 32:3; Kut 7:8—12:32; Isa 19:11 Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,
Katika nchi ya Misri, konde la Soani.
13 # Kut 14:21-22 Aliipasua bahari akawavusha;
Aliyasimamisha maji mfano wa chungu.
14 # Kut 13:21-22 Akawaongoza kwa wingu mchana,
Na usiku kucha kwa nuru ya moto.
15 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 105:41; Isa 41:18 Akapasua miamba jangwani;
Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.
16 # Kum 9:21 Akatokeza na vijito gengeni,
Akatelemsha maji kama mito.
17 # Ebr 3:16 Lakini wakazidi kumtenda dhambi,
Walipomwasi Aliye juu katika nchi ya kiu.
18 # Kut 16:2-15; Hes 11:4-23,31-35 Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao
Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao.
19 # Hes 11:4 Naam, walimwamba Mungu, wakasema,
Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?
20 # Kut 17:6; Hes 20:11 Tazama, aliupiga mwamba;
Maji yakabubujika, ikafurika mito.
Pia aweza kutupa chakula?
Atawaandalia watu wake nyama?
21Hivyo BWANA aliposikia akaghadhibika;
Moto ukawashwa juu ya Yakobo,
Hasira nayo ikapanda juu ya Israeli.
22 # Ebr 3:10 Kwa kuwa hawakumwamini Mungu,
Wala hawakuutumainia wokovu wake.
23 # Mwa 7:11; Kum 28:12 Lakini aliyaamuru mawingu juu;
Akaifungua milango ya mbinguni;
24 # Neh 9:15,20; Yn 6:31; 1 Kor 10:3 Akawanyeshea mana ili wale;
Akawapa nafaka ya mbinguni.
25Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;
Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.
26Aliuelekeza upepo wa mashariki mbinguni;
Akaiongoza kusi kwa uweza wake.
27Akawanyeshea nyama kama mavumbi,
Na ndege wenye mbawa,
Kama mchanga wa bahari.
28Akawaangusha kati ya matuo yao,
Pande zote za maskani zao.
29Wakala wakashiba sana;
Maana aliwaletea walivyovitamani;
30Hawakuachana na matakwa yao.
Ila chakula chao kikali ki vinywani mwao
31Hasira ya Mungu ikapanda juu yao,
Akawaua waliokuwa wanono;
Akawaangusha chini vijana wa Israeli.
32Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi,
Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.
33Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi,
Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha.
34 # Hes 5:15 Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;
Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.
35Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,
Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao.
36 # Eze 33:31 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,
Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
37 # Mdo 8:21 Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,
Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38 # Kut 34:6; Neh 9:17; Zab 86:15; 1 Fal 21:29; Isa 48:9; Mik 7:18; Rum 2:4 Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,
Husamehe uovu wala haangamizi.
Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,
Wala haiwashi hasira yake yote.
39 # Mwa 6:3; Yn 3:6; Yak 4:14; Ayu 7:7,16 Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili,
Upepo upitao wala haurudi.
40Walimwasi jangwani mara ngapi?
Na kumhuzunisha nyikani!
41Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu;
Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.
42Hawakuukumbuka mkono wake,
Wala siku ile alipowakomboa na mtesi.
43Alivyoziweka ishara zake katika Misri,
Na miujiza yake katika konde la Soani.
44 # Kut 7:17-21 Aligeuza damu mito yao,
Na vijito wasipate kunywa.
45 # Kut 8:1-6,20-24 Aliwapelekea mainzi wakawala,
Na vyura wakawaharibu.
46 # Kut 10:12-15 Akawapa tunutu mazao yao,
Na nzige kazi yao.
47 # Kut 9:22-25 Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe,
Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu.
48Akaacha ng’ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe,
Na makundi yao kwa umeme.
49 # Rum 2:8 Akawapelekea ukali wa hasira yake,
Ghadhabu, na uchungu, na taabu,
Kundi la malaika waletao mabaya.
50Akiifanyizia njia hasira yake;
Wala hakuziepusha roho zao na mauti,
Bali aliiachia tauni uhai wao;
51 # Mwa 9:22; Kut 12:29 Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri,
Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.
52 # Kut 13:17-22 Bali aliwaongoza watu wake kama kondoo,
Akawachunga kama kundi jangwani.
53 # Kut 14:26-28 Hao akawachukua salama wala hawakuogopa,
Bali bahari iliwafunikiza adui zao.
54 # Kut 15:17; Yos 3:14-17 Akawapeleka hadi mpaka wake mtakatifu,
Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume.
55 # Yos 11:16-23 Akawafukuza mataifa mbele yao,
Akawapimia urithi kwa kamba,
Na kuwakalisha kabila za Israeli katika hema zao.
56 # Amu 2:11-15 Lakini walimjaribu Mungu Aliye juu, wakamwasi,
Wala hawakuzishika shuhuda zake.
57 # Eze 20:27; Hos 7:16 Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao;
Wakaepea kama upinde usiofaa.
58 # Law 26:30; Hes 33:52; Kum 12:2 Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu,
Wakamtia wivu kwa sanamu zao.
59 # Ebr 4:13 Mungu akasikia, akaghadhibika,
Akamkataa Israeli kabisa.
60 # 1 Sam 4:11; Yer 7:12; Yos 18:1; Yer 7:12-14; 26:6 Akaiacha maskani ya Shilo,
Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu;
61 # 1 Sam 4:4-22; Amu 4:12 Akaziacha nguvu zake kutekwa,
Na fahari yake mkononi mwa mtesi.
62Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga;
Akaughadhibikia urithi wake.
63Moto ukawala vijana wao,
Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64 # Ayu 27:15 Makuhani wao walianguka kwa upanga,
Wala wajane wao hawakuomboleza.
65 # Isa 42:13 Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi,
Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo;
66Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma,
Akawatia aibu ya milele.
67Ila akaikataa hema ya Yusufu;
Wala hakuichagua kabila ya Efraimu.
68Bali aliichagua kabila ya Yuda,
Mlima Sayuni alioupenda.
69 # 1 Fal 6:1 Akajenga patakatifu pake kama vilele,
Kama dunia aliyoiweka imara milele.
70 # 1 Sam 16:11-12; 2 Sam 7:8; 1 Nya 17:7 Akamchagua Daudi, mtumishi wake,
Akamwondoa katika mazizi ya kondoo.
71 # 2 Sam 5:2; 1 Nya 11:2; Mik 5:2-4; Zek 11:4 Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa,
Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.
72 # 1 Fal 9:4 Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake,
Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 78: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha