Zaburi 40:16-17
Zaburi 40:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wote wale wanaokutafuta wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!” Mimi ni maskini na fukara, ee Bwana; lakini ee Bwana wewe wanikumbuka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; uje, ee Mungu wangu, usikawie!
Zaburi 40:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Washangilie na wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, BWANA ni Mkuu. Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Zaburi 40:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe BWANA. Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Zaburi 40:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “BWANA atukuzwe!” Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Bwana na anifikirie. Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; Ee Mungu wangu, usikawie.