Zaburi 38:1-22
Zaburi 38:1-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Mishale yako imenichoma; mkono wako umenigandamiza. Hamna mahali nafuu mwilini mwangu, kwa sababu umenikasirikia; hamna penye afya hata mifupani mwangu, kwa sababu ya dhambi yangu. Nimefunikwa kabisa na dhambi zangu, zinanilemea kama mzigo mzito mno kwangu. Madonda yangu yameoza na kunuka, na hayo ni matokeo ya ujinga wangu. Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viungo vyangu vimeshambuliwa na homa; mwilini mwangu hamna nafuu yoyote. Nimelegea na kupondekapondeka; nasononeka kwa kusongwa moyoni. Ee Bwana, wewe wajua tazamio langu lote; kwako hakikufichika kilio changu. Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia. Rafiki na wenzangu wanaepa kuona mateso yangu, na jamaa zangu wanakaa mbali nami. Wanaotaka kuniua wanatega mitego yao; wanaonitakia niumie wanatishia kuniangamiza. Mchana kutwa wanafanya mipango dhidi yangu. Lakini mimi nimekuwa kama kiziwi, sisikii; nimekuwa kama bubu asiyeweza kusema kitu. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, kama mtu asiye na chochote cha kujitetea. Lakini ninakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu; wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu. Nakuomba tu maadui wasinisimange, wasione fahari juu ya kuanguka kwangu. Karibu sana nitaanguka; nakabiliwa na maumivu ya daima. Naungama uovu wangu; dhambi zangu zanisikitisha. Maadui zangu hawajambo, wana nguvu; ni wengi mno hao wanaonichukia bure. Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu, wananipinga kwa sababu natenda mema. Usinitupe, ee Mwenyezi-Mungu; ee Mungu wangu, usikae mbali nami. Uje haraka kunisaidia; ewe Mwenyezi-Mungu, uliye wokovu wangu.
Zaburi 38:1-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu. Maana dhambi zangu zimenifunika kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno. Majeraha yangu yananuka na kutunga usaha, Kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kupondeka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unadundadunda, Nguvu zangu zimenitoka; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa. Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna ubishi kinywani mwake. Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu. Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza. Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima. Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu. Lakini walio adui zangu bila sababu wana nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi. Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nilifuata lililo jema. Wewe, BWANA, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.
Zaburi 38:1-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenipiga. Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. Maovu yangu yamenifunika kama mzigo mzito mno. Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani wangu wanakaa mbali nami. Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea kuhusu maangamizi yangu; hupanga hila mchana kutwa. Mimi ni kama kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake; nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. Ee BWANA, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wajitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.” Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote. Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu. Wengi wamekua adui zangu bila sababu; wale wanaonichukia bure ni wengi. Wanaolipa wema wangu kwa maovu hunisingizia ninapofuata lililo jema. Ee BWANA, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia.

Zaburi 38:1-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Naam, karibu zangu wamesimama mbali. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa. Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna hoja kinywani mwake. Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu. Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu. Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima. Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu. Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi. Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema. Wewe, BWANA, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.