Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 38

38
Ombi la Uponyaji kwa Anayejuta kwa Mateso
Zaburi ya Daudi, kwa matoleo ya kumbukumbu.
1Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako,
Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.
2Kwa maana mishale yako imenichoma,
Na mkono wako umenipata.
3Hamna uzima katika mwili wangu
Kwa sababu ya ghadhabu yako.
Wala hamna amani mifupani mwangu
Kwa sababu ya hatia zangu.
4Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa,
Kama mzigo mzito zimenilemea mno.
5Jeraha zangu zinanuka, zimeoza,
Kwa sababu ya upumbavu wangu.
6Nimepindika na kuinama sana,
Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika.
7 # Ayu 7:5 Maana viuno vyangu vimejaa homa,
Wala hamna uzima katika mwili wangu.
8Nimedhoofika na kuchubuka sana,
Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.
9Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako,
Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.
10Moyo wangu unapwita-pwita,
Nguvu zangu zimeniacha;
Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
11 # Lk 10:31 Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu;
Naam, karibu zangu wamesimama mbali.
12Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego;
Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya;
Na kufikiri hila mchana kutwa.
13Lakini kama kiziwi sisikii,
Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.
14Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,
Ambaye hamna hoja kinywani mwake.
15 # Yer 14:8 Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,
Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.
16Maana nalisema, Wasije wakanifurahia;
Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.
17Kwa maana mimi ni karibu na kusita,
Na maumivu yangu yako mbele yangu daima.
18 # Ayu 31:33; Zab 32:5; Mit 28:13; 2 Kor 7:9 Kwa maana nitaungama uovu wangu,
Na kusikitika kwa dhambi zangu.
19Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu,
Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.
20 # 1 Yoh 3:12; 1 Pet 3:13 Naam, wakilipa mabaya kwa mema,
Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.
21 # Zab 22:1,11 Wewe, BWANA, usiniache,
Mungu wangu, usijitenge nami.
22 # Kut 15:2; Isa 12:2 Ufanye haraka kunisaidia,
Ee Bwana, wokovu wangu.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 38: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha