Zaburi 37:4-6
Zaburi 37:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni. Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu. Ataufanya wema wako ungae kama mwanga, na uadilifu wako kama jua la adhuhuri.
Shirikisha
Soma Zaburi 37Zaburi 37:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumainie, naye atakutendea. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.
Shirikisha
Soma Zaburi 37Zaburi 37:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri.
Shirikisha
Soma Zaburi 37