Zaburi 37:3-7
Zaburi 37:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema, upate kuishi katika nchi na kuwa salama. Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni. Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu. Ataufanya wema wako ungae kama mwanga, na uadilifu wako kama jua la adhuhuri. Tulia mbele ya Mwenyezi-Mungu, mngojee kwa saburi; usihangaike juu ya wale wanaofanikiwa, watu wanaofaulu katika mipango yao mibaya.
Zaburi 37:3-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumainie, naye atakutendea. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri. Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Zaburi 37:3-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri. Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.
Zaburi 37:3-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtumaini BWANA na utende yaliyo mema. Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. Jifurahishe katika BWANA naye atakupa haja za moyo wako. Mkabidhi BWANA njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili: Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. Tulia mbele za BWANA na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.