Zaburi 37:23-25
Zaburi 37:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu, humlinda yule ampendezaye. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini, kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula.
Zaburi 37:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
Zaburi 37:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
Zaburi 37:23-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kama BWANA akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana BWANA humtegemeza kwa mkono wake. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula.