Zaburi 36:1-4
Zaburi 36:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Dhambi huongea na mtu mwovu, ndani kabisa moyoni mwake; jambo la kumcha Mungu halimo kabisa kwake. Mwovu hujipendelea mwenyewe, hufikiri uovu wake hautagunduliwa na kulaaniwa. Kila asemacho ni uovu na uongo; ameacha kutumia hekima na kutenda mema. Alalapo huwaza kutenda maovu, hujiweka katika njia isiyo njema, wala haachani na uovu.
Zaburi 36:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa. Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema. Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; hauchukii ubaya.
Zaburi 36:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. Kwa maana hujipendekeza machoni pake Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa. Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema. Huwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.
Zaburi 36:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kuna neno moyoni mwangu kutoka kwa Mungu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima au kutenda mema. Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya.