Zaburi 24:8-10
Zaburi 24:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, mwenye nguvu na uwezo; Mwenyezi-Mungu, mwenye uwezo vitani. Fungukeni enyi malango, fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu.
Zaburi 24:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Zaburi 24:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Zaburi 24:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA aliye na nguvu na uweza, ni BWANA aliye hodari katika vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA wa majeshi; yeye ndiye Mfalme wa utukufu.