Zaburi 24:5-7
Zaburi 24:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu, na haki yake kwa Mungu mwokozi wake. Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye; naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo. Fungukeni enyi milango; fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie.
Zaburi 24:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Zaburi 24:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Huyo atapokea baraka kutoka kwa BWANA, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta, wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia.

Zaburi 24:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)