Zaburi 24:3-6
Zaburi 24:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Nani atakayepanda mlima wa Mwenyezi-Mungu? Nani atakayekaa katika hekalu lake takatifu? Ni mtu wa matendo mema na moyo safi, asiyeuelekeza moyo wake katika upuuzi, wala kuapa kwa uongo. Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu, na haki yake kwa Mungu mwokozi wake. Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye; naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo.
Zaburi 24:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
Zaburi 24:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
Zaburi 24:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nani awezaye kuupanda mlima wa BWANA? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo. Huyo atapokea baraka kutoka kwa BWANA, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta, wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.