Zaburi 23:1-3,6
Zaburi 23:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu, na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani yake.
Zaburi 23:6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami, siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.
Zaburi 23:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Zaburi 23:6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Zab 23:6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.