Zaburi 22:8-11
Zaburi 22:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu. Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.
Zaburi 22:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Husema: “Alimtegemea Mwenyezi-Mungu, basi, Mungu na amkomboe! Kama Mungu anapendezwa naye, basi, na amwokoe!” Lakini ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, uliniweka salama kifuani pa mama yangu. Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu. Tangu nilipozaliwa wewe umekuwa Mungu wangu. Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia; wala hakuna wa kunisaidia.
Zaburi 22:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinisalimisha matitini mwa mama yangu. Kwako nilitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.
Zaburi 22:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu. Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.
Zaburi 22:8-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wanasema, “Amtegemea BWANA, basi BWANA na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.” Hata hivyo ulinitoa tumboni, ukanifanya nikutegemee, hata nilipokuwa ninanyonya matiti ya mama yangu. Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, toka tumboni mwa mama yangu umekuwa Mungu wangu. Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia.