Zaburi 22:11-23
Zaburi 22:11-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia; wala hakuna wa kunisaidia. Maadui wengi wanizunguka kama fahali; wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani! Wanafunua vinywa vyao kama simba, tayari kushambulia na kurarua. Nimekwisha kama maji yaliyomwagika; mifupa yangu yote imeteguka; moyo wangu ni kama nta, unayeyuka ndani mwangu. Koo langu limekauka kama kigae; ulimi wangu wanata kinywani mwangu. Umeniacha kwenye mavumbi ya kifo. Genge la waovu limenizunguka; wananizingira kama kundi la mbwa; wamenitoboa mikono na miguu. Nimebaki mifupa mitupu; maadui zangu waniangalia na kunisimanga. Wanagawana nguo zangu, na kulipigia kura vazi langu. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami; ewe msaada wangu, uje haraka kunisaidia. Iokoe nafsi yangu mbali na upanga, yaokoe maisha yangu makuchani mwa mbwa hao! Uniokoe kinywani mwa simba; iokoe nafsi yangu dhaifu toka pembe za nyati hao. Nitawasimulia ndugu zangu matendo yako; nitakusifu kati ya kusanyiko lao: Enyi mnaomcha Mwenyezi-Mungu, msifuni! Mtukuzeni enyi wazawa wote wa Yakobo! Mcheni Mungu enyi wazawa wote wa Israeli!
Zaburi 22:11-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi. Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, BWANA, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa. Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazawa wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazawa wa Israeli.
Zaburi 22:11-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi. Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, BWANA, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa. Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
Zaburi 22:11-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia. Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. Simba wanaonguruma na kurarua mawindo wanapanua vinywa vyao dhidi yangu. Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imeteguka viungoni. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu. Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo. Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira; wamenidunga mikono na miguu. Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga. Wanagawana nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura. Lakini wewe, Ee BWANA, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie. Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za nyati. Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. Ninyi ambao mnamcha BWANA, msifuni! Ninyi nyote wazao wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wa Israeli!