Zaburi 22:1-6
Zaburi 22:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Mbona uko mbali sana kunisaidia, mbali na maneno ya kilio changu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu; napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati. Hata hivyo, wewe ni mtakatifu; wewe watawala na kusifiwa na Waisraeli. Wazee wetu walikutegemea; walikutegemea, nawe ukawaokoa. Walikulilia wewe, wakaokolewa; walikutegemea, nao hawakuaibika. Lakini mimi ni mdudu tu, wala si mtu; nimepuuzwa na kudharauliwa na watu.
Zaburi 22:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. Lakini Wewe U Mtakatifu, Utukuzwaye na sifa za Israeli. Baba zetu walikutumainia Wewe, Walitumainia, na Wewe ukawaokoa. Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumainia, nao hawakuaibika. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Nimedharauliwa na kupuuzwa na watu.
Zaburi 22:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.
Zaburi 22:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi. Hata hivyo umesimikwa kwenye kiti cha enzi, Wewe Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli. Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa. Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika. Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.