Zaburi 21:1-7
Zaburi 21:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako, anafurahi mno kwa msaada uliompa. Umemtimizia matakwa ya moyo wake; wala hukumkatalia ombi lake. Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri; umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake. Alikuomba maisha nawe ukampa; ulimpa maisha marefu milele na milele. Kwa msaada wako ametukuka sana; wewe umemjalia fahari na heshima. Wamjalia baraka zako daima; wamfurahisha kwa kuwako kwako. Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.
Zaburi 21:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake. Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika.
Zaburi 21:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. Kwa kuwa mfalme humtumaini BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.
Zaburi 21:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee BWANA, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi furaha yake ilivyo kuu kwa ushindi unaompa! Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake. Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake. Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu. Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako. Kwa kuwa mfalme anamtumaini BWANA; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.