Zaburi 19:1-4
Zaburi 19:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga ladhihirisha kazi ya mikono yake. Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Hamna msemo au maneno yanayotumika; wala hakuna sauti inayosikika; hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote, na maneno yao yafika kingo za ulimwengu. Mungu ameliwekea jua makao yake angani
Zaburi 19:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Hakuna usemi wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema
Zaburi 19:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema
Zaburi 19:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake. Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki. Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.