Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 19

19
Utukufu wa Mungu katika Viumbe na Hukumu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Isa 40:22; Rum 1:19 Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
2Mchana husemezana na mchana,
Usiku hutolea usiku maarifa.
3Hakuna lugha wala maneno,
Sauti yao haisikilikani.
4 # Rum 10:18 Sauti yao imeenea duniani mwote,
Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Katika hizo ameliwekea jua hema,
5 # Mhu 11:7 Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,
Lafurahi kama mtu aliye hodari
Kwenda mbio katika njia yake.
6 # Mhu 1:5 Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu,
Na kuzunguka kwake hata miisho yake,
Wala kwa hari yake
Hakuna kitu kilichositirika.
7Sheria ya BWANA ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa BWANA ni amini,
Humtia mjinga hekima.
8 # Neh 9:13; Rum 7:12 Maagizo ya BWANA ni ya adili,
Huufurahisha moyo.
Amri ya BWANA ni safi,
Huyatia macho nuru.
9Kicho cha BWANA ni kitakatifu,
Kinadumu milele.
Hukumu za BWANA ni kweli,
Zina haki kabisa.
10Ni za kutamanika kuliko dhahabu,
Kuliko wingi wa dhahabu safi.
Nazo ni tamu kuliko asali,
Kuliko sega la asali.
11 # Mit 6:22,23 Tena mtumishi wako huonywa kwazo,
Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.
12Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?
Unitakase na mambo ya siri.
13Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi,
Yasinitawale mimi.
Ndipo nitakapokuwa kamili,
Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.
14 # Isa 44:6 Maneno ya kinywa changu,
Na mawazo ya moyo wangu,
Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA,
Mwamba wangu, na mwokozi wangu.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 19: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha