Zaburi 18:30-36
Zaburi 18:30-36 Biblia Habari Njema (BHN)
Huyu Mungu matendo yake hayana dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia usalama. Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu? Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu? Mungu ndiye anijaliaye nguvu kila upande; ndiye anayeifanya salama njia yangu. Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Hunifunza kupigana vita, mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba. Umenipa ngao yako ya kuniokoa; mkono wako wa kulia umenitegemeza; wema wako umenifanikisha. Umenirahisishia njia yangu; wala miguu yangu haikuteleza.
Zaburi 18:30-36 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia. Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Anaifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezipanulia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.
Zaburi 18:30-36 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia. Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.
Zaburi 18:30-36 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la BWANA halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya BWANA? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua. Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.