Zaburi 145:1-10
Zaburi 145:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako. BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Zaburi 145:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitakutukuza, ee Mungu wangu na mfalme wangu; nitalitukuza jina lako daima na milele. Nitakutukuza kila siku; nitalisifu jina lako daima na milele. Mwenyezi-Mungu ni mkuu, astahili sifa nyingi; ukuu wake hauwezi kuchunguzika. Kizazi hata kizazi, sifa za matendo yako zitasimuliwa, watu watatangaza matendo yako makuu. Nitanena juu ya utukufu na fahari yako, nitayatafakari matendo yako ya ajabu. Watu watatangaza ukuu wa matendo yako ya ajabu, nami nitatangaza ukuu wako. Watatangaza sifa za wema wako mwingi, na kuimba juu ya uadilifu wako. Mwenyezi-Mungu ni mwenye huruma na rehema; hakasiriki ovyo, amejaa fadhili. Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wote, ni mwenye huruma kwa viumbe vyake vyote. Viumbe vyako vyote vitakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, nao waaminifu wako watakutukuza.
Zaburi 145:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hauchunguziki. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti. BWANA ni mwenye fadhili na huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba. Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Zaburi 145:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako. BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Zaburi 145:1-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe kuhusu haki yako. BWANA ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. BWANA ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya. Ee BWANA, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.