Zaburi 14:1-3
Zaburi 14:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema! Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Lakini wote wamekosa, wote wamepotoka pamoja; hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja.
Zaburi 14:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Zaburi 14:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Zaburi 14:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema. BWANA anawachungulia wanadamu kutoka mbinguni aone kama kuna mwenye hekima, yeyote anayemtafuta Mungu. Wote wamepotoka, wote wameoza pamoja; hakuna atendaye mema, naam, hakuna hata mmoja!