Zaburi 14:1-2 - Compare All Versions
Zaburi 14:1-2 BHN (Biblia Habari Njema)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema! Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.
Zaburi 14:1-2 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.
Zaburi 14:1-2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.
Zaburi 14:1-2 NEN (Neno)
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema. BWANA anawachungulia wanadamu kutoka mbinguni aone kama kuna mwenye hekima, yeyote anayemtafuta Mungu.