Zaburi 119:91-93
Zaburi 119:91-93 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa amri yako viumbe vyote vipo leo, maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningalikwisha angamia kwa taabu zangu. Sitasahau kamwe kanuni zako, maana kwa hizo umenipa uhai.
Zaburi 119:91-93 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika mateso yangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha.
Zaburi 119:91-93 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika taabu zangu. Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha.